ESKi Tanzania ni programu ya kukuza uwezo iliyoundwa ili kukuza na kuendeleza kizazi kipya cha viongozi, watetezi wa jamii na wataalamu wanaoshughulika na utawala wa sekta ya madini, mafuta na gesi ili kuimarisha sauti za wananchi katika kuboresha sera na taratibu zinazosimamia sekta ya madini, mafuta na gesi.
Programu hii inakusudia kuwajengea uwezo viongozi na wataalamu wanaoibuka ambao wana maarifa na uzoefu mdogo katika utawala wa sekta ya madini, mafuta na gesi. Aidha, inalenga kutoa maarifa, ujuzi, na zana za msingi ili kuboresha ushirikiano wao na viongozi wa sekta, watunga sera, na wadau wengine muhimu kuhusu usimamizi wa sekta ya madini, mafuta, na gesi asilia nchini Tanzania.
Programu hii inajumuisha mafunzo ya kanuni za msingi na dhana kuu za sekta ya madini,mafuta na gesi utawala na uwazi, usimamizi wa mapato, athari za haki za binadamu, usimamizi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi, athari za kijinsia, pamoja na madini muhimu na mpito wa nishati.
ADA
Kozi hii ni bure na haitahitaji ada yoyote kwa ushiriki.
MAHITAJI YA MWOMBAJI
Mwombaji anapaswa kuwa na:
- Uelewa wa msingi kuhusu sekta ya madini, mafuta na gesi.
- Uzoefu wa angalau miezi sita katika sekta ya madini, mafuta na gesi. Yaani, utawala, usimamizi wa mazingira, maendeleo ya jamii, au sekta zinazohusiana.
- Uwezo wa kuzungumza na kuandika kwa Kiswahili au Kingereza.
- Upatikanaji wa kuhudhuria siku zote za programu kukamilisha kozi nzima.
- Mwombaji anatarajiwa kuwa na mahali, shirika, au taasisi inayohusiana na sekta ya madini, mafuta na gesi ambapo anaweza kutumia maarifa atakayoyapata.
NAMNA YA KUENDESHA PROGRAMU
Programu itafanyika Dar es Salaam, na itadumu kwa siku tano mfululizo, kuanzia tarehe 16 hadi 20 Septemba 2024.
NAMNA YA KUOMBA
Waombaji wanaostahili wanapaswa kutuma maombi yao kwa m.ally@hakirasilimali.or.tz na kunakili kwa lshao@hakirasilimali.or.tz kabla ya tarehe 14 Agosti 2024. Wakiambatanisha viambatanisho vifuatavyo.
- Barua ya motisha ya ukurasa mmoja. (Motivational letter)
- Wasifu wa kitaaluma (sio zaidi ya kurasa 2) ukionyesha uzoefu katika sekta ya nishati au madini. (CV)
- Nakala ya Kitambulisho cha Taifa au Kitambulisho chochote halali.
- Barua ya mapendekezo. (Recommendation letter)